BABA wa kocha wa Manchester United, Jose Mourinho aliyekuwa anafahamika kwa jina la Jose Manuel Mourinho Felix, amefariki dunia Jumapili na tayari mwanawe huyo yuko Ureno kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika leo.
Mourinho ameonekana na marafiki akiwa msibani mjini Setubal leo akiwa mwenye huzuni baada ya msiba huo mzito.
Jose Manuel Mourinho Felix, ambaye amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya kwa miezi kadhaa, amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 79 mjini Setubal jana na atazikwa kesho.
Enzi zake, Mourinho Felix alizichezea Victoria Setubal na Belenenses, akicheza jumla ya mechi 274 katika Ligi Kuu ya Ubelgiji kuanzia mwaka 1955 hadi 1974.
Jose Mourinho (kushoto) akiwa na baba yake ambaye alicheza mechi zaidi ya 250 katika Ligi Kuu ua Ureno kabla ya kuwa kocha PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Alipata nafasi pia ya kuichezea mechi moja timu ya taifa ya Ureno, akitokea benchi dakika za mwishoni dhidi ya Jamhuri ya Ireland mwaka 1972 katika michuano ya Kombe la Uhuru Brazil.
Baada ya kutundika glavu zake, Mourinho Felix akafundisha klabu kadhaa Ureni zikiwemo Uniao Leiria, Amora, Rio Ave, Belenenses na Vitoria.
Jose Mourinho, aliyekuwa anamtembelea baba yake mara ka mara kumjulia hali akiwa mgonjwa, amehuzunishwa mno na msiba huo, ambao ni wa familia nzima ya soka Ureno.
0 comments:
Post a Comment