MSHAMBULIAJI Mohamed Salah yuko mbioni kujiunga na Liverpool kwa dau la rekodi la Pauni Milioni 39.
Salah alisafiri kwenda Merseyside Jumanne kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya kuelekea kurejea Ligi Kuu ya England.
Usajili wa winga huyo wa zamani wa Chelsea umekuwa kipaumbele Liverpool na mazungumzo yamekuwa yakiendelea na klabu yake ya sasa, AS Roma tangu mwezi uliopita.
Klabu hiyo ya Italia ilikataa dau la Pauni Milioni 28 kumuuza Mmisri huyo mwanzoni mwa Juni, lakini makubaliano yamefikiwa kwa sasa na Salah anakaribia kumpiku Andy Carroll kama mchezaji ghali kuwahi kusajiliwa na klabu hiyo.
Salah, ambaye alipata fursa ya kujiunga na Liverpool miaka mitatu iliyopita, lakini akavchagua kuendelea kufanya kazi na Jose Mourinho klabu ya Chelsea, amekubali mshahara wa Pauni 90,000 kwa wiki.
0 comments:
Post a Comment