KIUNGO wa timu ya taifa ya Ethiopia, Gatoch Panom amejiunga na Anzhi Makhackala ya Urusi kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka Coffee ya Ligi Kuu ya nchini mwake.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alikwenda Moscow Jumatano wiki iliyopita kwa majaribio katika klabu ya Anzhi na sasa amefuzu vipimo vyake vya afya bila tatizo.
Taarifa ya wakala wake, David Beshah imesema kwamba amefanya mazungumzo na klabu hiyo na makubaliano yamefikiwa, siku tano baada ya majaribio yake Anzhi.
"Tumefurahishwa mno na jambo hili. Ana kipaji sana na nilijua atachukuliwa na Anzhi,”alisema Beshah.
Gatoch Panom (kulia) amejiunga na Anzhi Makhackala ya Urusi kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka Coffee ya Ligi Kuu ya Ethiopia
Gatoch sasa ataongozana na kikosi cha Anzhi kwenda Slovenia wiki ijayo kuanza maandalizi ya msimu mpya kwa kambi itakayohusisha pia ni mechi za kirafiki.
Anzhi yeenye maskani yake Dagestan imewahi kuwa na wachezaji wakubwa duniani, akiwemo Mwanasoka Bora wa zamani Afrika, Samuel Eto’o wa Cameroon, beki wa zamani wa Brazil, Roberto Carlos na Christopher Samba wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Gatoch alifunga mabao manane katika Ligi Kuu ya Ethiopia (EPL) na hivi karibuni aliichezea mechi yake ya 27 timu yake ya taifa, Walia Ibex’s dhidi ya Ghana kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika.

0 comments:
Post a Comment