Manchester United imekamilisha usajili wa beki wa Benfica, Victor Lindelof PICHA ZAIDI GONGA HAPA
TIMU ya Manchester United imekamilisha usajili wa beki Victor Lindelof mwenye urefu wa futi sita kutoka Benfica ya Ureno baada ya kufuzu vipimo vya afya.
Lindelof, ambaye ameigharimu United Pauni Milioni 30.7, aliwasili viwanja vya mazoezi vya klabu, Carrington Jumatanop asubuhi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa akisakwa na kocha wa United, Jose Mourinho kwa muda mrefu.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Sweden ameelezea furaha yake kutua Old Trafford.
Inafahamika pia Benfica inaweza kupata Pauni Milioni 8.8 zaidi.
Katika mahojiano na tovuti rasmi ya klabu, amesema: "Nina furaha kujiunga na Manchester United. Nimefurahia wakati wangu nikiwa Benfica na nimejifunza mengi huko. Lakini naangalia mbele namna ya kucheza Ligi Kuu nikiwa Old Trafford na Jose Mourinho,"amesema.
Mchezaji anatarajiwa kuanza kujumuika kucheza na wachezaji wenzake wapy katika ziara ya Marekani kujiandaa na msimu na Mourinho anaamini Lindelof ataongeza tija katika katika safu yake ya ulinzi hususan baada ya timu kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa.
0 comments:
Post a Comment