Na Mwandishi Wetu, RUSTERNBURG
TANZANIA imeanza vyema michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) baada ya ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa Kundi A dhidi ya Malawi jioni ya leo Uwanja wa Moruleng mjini Rusternburg, Afrika Kusini.
Shukrani kwake winga wa Simba SC ya nyumbani, Shiza Ramadhani Kichuya aliyefungua vizuri akaunti yake ya mabao Taifa Stars kwa kufunga mabao yote hayo kipindi cha kwanza, dakika ya 13 na 18.
Mabao yaa Kichuya, mshindi wa tuzo ya Bao Bora Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita, yanamfanya kocha Salum Shaaban Mayanga aandike ushindi wa tatu katika mechi nne tangu aanze kuifundisha Taifa Stars Machi mwaka huu, akimpokea Mtanzania mwenzake, Charles Boniface Mkwasa.
Shiza Kichuya (kulia) amefunga mabao yote Taifa Stars ikiilaza Malawi 2-0 leo Kombe la COSAFA
Tanzania kutoka Mashariki mwa Afrika, inashiriki kama mwalikwa hii ikiwa mara ya tatu na mara ya pili mfululizo baada ya mwaka jana, kufuatia kucheza kwa mara ya kwanza mashindano hayo mwaka 1996t.
Na mbali na Tanzania na Malawi, timu nyingine katika Kundi A ni Mauritius na Angola zinazomenyana kuanzia Saa 12:00 jioni hii hapo hapo Moruleng. Kundi B lina timu za Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe na mshindi wa kwanza wa kila kundi atakwenda moja kwa moja hatua ya Robo Fainali. Botswana, Zambia na Afrika Kusini, Namibia, Lesotho na Swaziland zimefuzu moja kwa moja Robo Fainali.
Kocha Mayanga anaitumia michuano hii kama sehemu ya maandalizi ya mchezo wake wa kwanza wa kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), michuano inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.
Taifa Stars itaanza na Rwanda, mchezo wa kwanza ukichezwa Julai 15 Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, kabla ya kurudiana mjini Kigali Julai 21, mwaka huu.
Kikosi cha Tanzania leo kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe/Hassan Kessy, Gardiel Michael, Abdi Banda, Salim Mbonde, Erasto Nyoni, Himid Mao, Shiza Kichuya, Simon Msuva, Muzamil Yasssin, Elias Maguri/Mbaraka Yussuf dk62.

0 comments:
Post a Comment