TIMU ya Manchester City inatarajiwa kuanza mazungumzo rasmi na beki Dani Alves baada ya Juventus kuthibitisha itavunjiana naye mkataba.
Beki huyo wa kulia mwenye umri wa miaka 34 anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili na City akaungane na kocha wake wa zamani, Pep Guardiola walipokuwa Barcelona akivunja mkataba na Juventus.
Akizungumza na Calciomercato.com na Mediaset Premium, Mtendaji Mkuu wa Juventus, Beppe Marotta alisema: "Si uvunjaji wa mkataba kwa utashi wetu, bali matakwa ya mchezaji mwenyewe,".
Dani Alves atavunja mkataba wake na Juventus ili ahamie Man Cit akaungane tena na kocha wake wa zamani, Pep Guardiola PICHA ZAIDI GONGA HAPA
"Dani Alves ametuambia anataka kujaribu uzoefu mwingine, hivyo atavunja mkataba kwa makubaliano ya kiungwana na tunamtakia kila la heri,".
"Ni kweli kuliwa kuna mambo ya kustaajabisha katika mazungumzo yake, lakini tunathibitisha hakukuwa na mgawanyiko,"alisema.
City imesema ilitaka kumuuza Nolito na wamesema Sevilla wapo karibu kumchukua kwa mkopo mshambuliaji huyo.
0 comments:
Post a Comment