Robert Lewandowski alikasirishwa na wachezaji wenzake kutompa sapiti mwishoni mwa msimu akiwania ufungaji bora wa BUndesliga PICHA ZAIDI GONGA HAPA
KLABU ya Bayern Munich imewaonya wapinzani wanaotaka kumchukua mshambuliaji wao Robert Lewandowski, kwamba wataadhibiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Chelsea na Manchester United zote zimeripotiwa kumfiatilia mwanasoka huyo wa kimataifa wa Poland huku ikiamini na tayari zimekwishawasiliana na wakala wa Lewandowski, ambaye amesema mteja wake hakuwa na furaha.
Taarifa ya klabu hiyo imesema: "Mkataba wa Lewandowski unamalizika mwaka 2021, alisaini si muda mrefu uliopita. Lewandowski hataki kuondoka Bayern. Hakuna mazungumzo na klabu nyingine na haiwezi kuwa yoyote. Ikiwa klabu nyingine zinazungumza na mchezaji mwenye mkataba mrefu zinajihatarisha kuadhibiwa na FIFA," imesema taarifa hiyo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 inafahamika hana furaha Bayern na wakala wake, Maik Barthel amesema kwamba uongozi na wachezaji wenzake hawakumpa sapoti ya kutosha mwishoni mwa msimu wakati anapigania ufungaji bora na alicheza licha ya kuwa na maumivu ya bega.
Lewandowski aliongeze mkataba Desemba mwaka jana hadi mwaka 2021 na mbali na Chelsea na Man United, klabu nyingine inayotajwa kumuhitaji ni Real Madrid.
0 comments:
Post a Comment