MCHEZAJI wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka ya Zambia, Emmanuel Banda ameondoka klabu ya Sporting Esmoriz ya Ureno na kujiunga na KV Oostende ya Ubelgiji.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 19, amesaini mkataba wa miaka mitatu na timu hiyo ya Ligi Kuu ya Ubelgiji ambao utamuweka huko hadi mwaka 2020.
Banda kuhamia Ubelgiji ni pigo kwa vigogo wa Ligi Kuu ya Misri, Zamalek ambao walikuwa wanamtaka nyota huyo chipukizi.
Banda akikabidhiwa jezi ya KV Oostende baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu kutoka Esmoriz ya Ureno
Ilishindikana Banda kwenda Misri baada ya klabu ya Esmoriz kutaka ada ya uhamisho ya Pauni 300,000 mwezi Januari, fedha ambazo 'The Whites' hawakuwa tayari kulipa.
Tayari KV Oostende imethibitisha kumsaini mchezaji huyo kupitia kurasa zao mbalimbali za mitandao ya kijamii. Wakati huo huo, Banda amethibitisha uhamisho huo kupitia video aliyoposti kwenye akaunti yake Twiiter.
Emmanuel Banda alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya vijana ya Zambia kilichotwaa ubingwa wa U-20 barani Afrika katika fainali ambazo wao walikuwa wenyeji, kabla ya kwenda kufika Robo Faiali kwenye Kombe la Dunia mwezi Mei, ambako alifunga bao dhidi ya Ujerumani hatia ya 16 Bora akiiwezesha Zambia kuwang'oa 'Die Mannschaft' kwenye mashindano.
0 comments:
Post a Comment