KLABU ya Arsenal imewaahidi posho nzuri ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wachezaji wake nyota, Alexis Sanchez na Mesut Ozil ili kuwavutia wasaini mikataba mipya.
The Gunners, ambao wapo mbioni kumsajili mshambuliaji wa Monaco, Thomas Lemar, bado haijamaliza tatizo la mgomo wa kusaini mikataba mipya kwa wachezaji wake hao wawili waliobakiza mwaka mmoja.
Arsenal imewapa ofa nyota hap wawili ya asilimia 20 zaidi katika posho zao za Ligi ya Mabingwa ili wasaini mikataba mipya.
Nyongeza ya mishahara itawekwa pale tu Arsenal itakaporejesha hadhi yake katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mesut Ozil (kushoto) na Alexis Sanchez wote wanataka mishahara ya Pauni 300,000 kwa wiki kila mmoja ili wasaini mikataba mipya Arsenal PICHA ZAIDI GONGA HAPA
The Gunners wameshindwa kufuzu kwenye michuano hiyo mikubwa ya klabu Ulaya kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 20 msimu uliopita baada ya kumaliza nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England.
Sanchez na Ozil wote walikataa mishahara mipya ya Pauni 250,000 kwa wiki wakiwa wanelekea mwaka wa mwisho wa mikataba yao na wote walitaka Pauni 300,000, ambazo klabu hiyo haikuwa tayari kutoa.
Lakini kwa sasa klabu inajiandaa kuwalipa wachezaji hao wawili kiasi kinachikaribiana na walichoomba kama watasaini mikataba mipya na kuisaidia The Gunners kumaliza ndani ya nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
0 comments:
Post a Comment