// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TSHABALALA MCHEZAJI BORA LIGI KUU MEI, AWABWAGA NIYONZIMA NA SHAABAN IDDI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TSHABALALA MCHEZAJI BORA LIGI KUU MEI, AWABWAGA NIYONZIMA NA SHAABAN IDDI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, May 22, 2017

    TSHABALALA MCHEZAJI BORA LIGI KUU MEI, AWABWAGA NIYONZIMA NA SHAABAN IDDI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BEKI wa Simba SC, Mohamed Hussein 'Tshabalala' amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzaniua Bara wa mwezi Mei kwa msimu wa 2016/2017.
    Hussein aliwashinda wachezaji Haruna Niyonzima wa Yanga na Shabani Idd wa Azam FC. 
    Katika mwezi Mei kulikuwa na raundi tatu ambazo Hussein alicheza kwa dakika zote 270 na kutoa mchango mkubwa katika kuisadia timu yake kubaki katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom.
    Pia alionesha nidhamu ya hali ya juu, hivyo kutopewa onyo la aina yoyote.
    Mohammed Hussein 'Tshabalala' ndiye mchezaji bora wa Ligi Kuu mwezi Mei

    Kwa kushinda tuzo hiyo, Kaseja atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania.
    Wachezaji wengine walioshinda tuzo za mwezi za Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/2017 ni John Bocco wa Azam (Agosti), Shiza Kichuya wa Simba (Septemba), Simon Msuva wa Yanga (Oktoba) na Riphat Said wa Ndanda (Novemba).
    Wengine ni Method Mwanjali wa Simba (Desemba), Juma Kaseja wa Kagera Sugar (Januari), Hassan Kabunda wa Mwadui (Februari), Mbaraka Yusuf wa Kagera Sugar (Machi) na Abdulrahman Musa wa Ruvu Shooting (Aprili).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TSHABALALA MCHEZAJI BORA LIGI KUU MEI, AWABWAGA NIYONZIMA NA SHAABAN IDDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top