// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA WAPEWA BARUA KUJULISHWA KUPOKONYWA POINTI ZA KAGERA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA WAPEWA BARUA KUJULISHWA KUPOKONYWA POINTI ZA KAGERA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, May 06, 2017

    SIMBA WAPEWA BARUA KUJULISHWA KUPOKONYWA POINTI ZA KAGERA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BODI ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imewajibu rasmi Simba SC juu ya kupokonywa pointi tatu za mezani walizopewa baada ya rufaa yao dhidi ya Kagera Sugar mwezi uliopita.
    Simba ilifungwa 2-1 na Kagera Sugar Aprili 2, mwaka huu Uwanja wa Kaitaba, Bukoba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Hata hivyo, baada ya mchezo huo, Simba ikakata rufaa Bodi ya Ligi ikidai Kagera Sugar walimchezesha kimakosa beki Mohammed Fakhi kwa sababu alikuwa ametoka kuonyeshwa kadi tatu za njano.
    Simba ilifungwa 2-1 na Kagera Sugar Aprili 2, mwaka huu Uwanja wa Kaitaba, Bukoba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 
    Bodi ya Ligi ikalipeleka suala hilo Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi, maarufu kama Kamati ya Saa 74 ambayo iliipa ushindi Simba.
    Hata hivyo, Kagera Sugar wakapeleka malalamiko yao TFF wakidai mchezaji wao hakuwa na kadi tatu na Kikao cha Kamati ya Katiba Sheria na Hadhi za Wachezaji kikabatilisha maamuzi ya Kamati ya Saa 72 na matokeo ya Uwanjani yakabaki kama yalivyokuwa.
    Lakini wiki hii, Rais wa Simba, Evans Aveva akasema wanataka kusonga mbele kudai haki yao, lakini wanashindwa kwa sababu hawajapewa barua ya maamzi hayo.
    Na kukata mzizi wa fitina, leo Bodi kupitia kwa Mwenyekiti wake, Hamad Yahya imeipa barua Simba kuwataarifu kuwa wamepokonywa pointi za mezani.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA WAPEWA BARUA KUJULISHWA KUPOKONYWA POINTI ZA KAGERA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top