Kiungo wa Chelsea, Mfaransa N'Golo Kante mwenye umri wa miaka 26 akiwa ameshika tuzo yake ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Ligi Kuu ya England baada ya kukabidhiwa jana kufuatia kuwapiku wachezaji wenzake wa The Blues, Eden Hazard na Cesar Azpilicueta, nyota watatu wa Tottenham Hotspur, Harry Kane, Dele Alli na Jan Vertonghen, Romelu Lukaku wa Everton na Alexis Sanchez wa Arsenal.
Hiyo inakuwa tuzo ya tatu msimu huu kwa mchezaji huyo aliyejiunga na Chelsea msimu huu na kuipa ubingwa wa Ligi Kuu akitoka Leicester City aliyoipa taji hilo msimu uliopita, kwani tayari ameshinda tuzo za Mchezaji Bora wa Mwaka wa Chama cha Waandishi wa Soka na Mchezaji Bora wa Mwaka na Chama cha Wachezaji wa Kulipwa PICHA ZAIDI GONGA HAPA

0 comments:
Post a Comment