// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MBARAKA YUSSUF: CHIPUKIZI MWENYE NDOTO ZA KUFIKA MBALI KISOKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MBARAKA YUSSUF: CHIPUKIZI MWENYE NDOTO ZA KUFIKA MBALI KISOKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, May 04, 2017

    MBARAKA YUSSUF: CHIPUKIZI MWENYE NDOTO ZA KUFIKA MBALI KISOKA

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    MIONGONI mwa wachezaji wanaofanya vizuri msimu huu katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ni mshambuliaji chipukizi, Mbaraka Yussuf Abeid wa Kagera Sugar ya Bukoba.
    Huyo ni mfungaji wa bao la ushindi la timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ikiilaza 2-1 Burundi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa Machi 28, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambaye anawania ufungaji bora wa Ligi Kuu kwa sasa akichuana na Simon Msuva wa Yanga na Shiza Kichuya wa Simba.
    Hivi karibuni, Bin Zubeiry Sports – Online ilifanya mahojiano na mchezaji huyo aliyeibukia katika kikosi cha timu ya vijana cha Simba mjini Dar es Salaam, kabla ya kwenda Bukoba. Endelea.
    Mbaraka Yussuf (kulia) akiwatoka mabeki wa Simba Aprili 2, mwaka huu Uwanja wa Kaitaba, Bukoba 
    Bin Zubeiry Sports – Online: Mambo vipi straika
    Mbaraka Yussuf Abeid: Safi tu bro, karibu
    Bin Zubeiry Sports – Online: Asante, nimekuja kwa ahadi yetu ya mahojiano. Uko tayari?
    Mbaraka Yussuf Abeid: Hakuna shaka, tuendelee tu kaka.
    Bin Zubeiry Sports – Online: vipi mkataba wako unaisha lini Kagera Sugar                        
    Mbaraka Yussuf: Mwisho wa msimu huu
    Bin Zubeiry Sports – Online: Ina maana umebakiza miezi michache tu                        
    Mbaraka Yussuf: Yah                        
    Bin Zubeiry Sports – Online: Vipi Simba una mkataba nao wowote?
    Mbaraka Yussuf: Hapana                        
    Bin Zubeiry Sports – Online: Yanga wakikutaka vipi
    Mbaraka Yussuf: Mimi nipo tayari kucheza timu yoyote kama wakinikidhia mahitaji yangu               
    Bin Zubeiry Sports – Online: Una uhusiano wowote na kipa wa zamani wa Pamba ya Mwanza, Yussuf Abeid
    Mbaraka Yussuf: Hapana.
    Bin Zubeiry Sports – Online:  Baba yako yuko wapi
    Mbaraka Yussuf: Kafariki                        
    Bin Zubeiry Sports – Online: Pole sana. Lini?                        
    Mbaraka Yussuf: Tangu mwaka 2010                        
    Bin Zubeiry Sports – Online: Alikuwa anaishi wapi 
    Mbaraka Yussuf: Kinondoni
    Bin Zubeiry Sports – Online: Kwa hiyo wewe umezaliwa Dar es Salaam?                        
    Mbaraka Yussuf: Yah                        
    Bin Zubeiry Sports – Online: Ulizaliwa lini                         
    Mbaraka Yussuf: Septemba 2 mwaka 1997                        
    Bin Zubeiry Sports – Online: Shule ya Msingi umesoma wapi
    Mbaraka Yussuf: Kumbukumbu                        
    Bin Zubeiry Sports – Online: Sekondari                        
    Mbaraka Yussuf: Nilianzia Tabata, Nikahamia Kinondoni Muslim
    Bin Zubeiry Sports – Online: Umesoma hadi kidato cha ngapi
    Mbaraka Yussuf: Cha nne tu
    Bin Zubeiry Sports – Online: Soka ulianzia wapi 
    Mbaraka Yussuf: Kinondoni Muslim                        
    Bin Zubeiry Sports – Online: Timu ya kwanza ya mtaani kuchezea ni ipi?                        
    Mbaraka Yussuf: Vijana Muslim
    Bin Zubeiry Sports – Online: Timu nyingine ulizochezea za mtaani ni zipi                        
    Mbaraka Yussuf: Hakuna                        
    Bin Zubeiry Sports – Online: Ndondo ulikuwa huendi kupiga
    Mbaraka Yussuf: Siyo sana                        
    Bin Zubeiry Sports – Online: Simba uliingia lini
    Mbaraka Yussuf: Mwaka 2014                        
    Bin Zubeiry Sports – Online: Ulicheza timu B tu, au uliwahi kupandishwa?                        
    Mbaraka Yussuf: Nilicheza B, nikapandishwa timu kubwa, nikajiandaa nao pre season kule Lushoto (mwaka juzi). Nikaenda nao Zanzibar, kabla Ligi kuunza ndiyo wakanipeleka Kagera kwa mkopo ambako nilianza kucheza msimu uliopita, mkopo ukaisha msimu huu nimesaini mkataba wangu mwenyewe sasa 
    Bin Zubeiry Sports – Online: Unawakumbuka uliokuwa nao Simba B ambao nao sasa hivi wanawika Ligi Kuu
    Mbaraka Yussuf: Labda ninamkumbuka mmoja yule kipa Dennis (Richard) yeye ndiyo yupo SImba sasa hivi timu kubwa nay eye. Wengine sijui wapo timu gani kwa sasa 
    Bin Zubeiry Sports – Online: Umewahi kuchezea timu za vijana za taifa?                        
    Mbaraka Yussuf: Hapana                        
    Bin Zubeiry Sports – Online: Kwa Sasa unachuana na akina na Msuva na Kichuya kwenye mbio za ufungaji bora wa Ligi Kuu, unadhani utaweza kuwapiku hao?
    Mbaraka Yussuf: Hakuna jambo lisililowezekana. Cha muhimu ni juhudi tu. Kama siyo msimu huu, basi msimu mwingine nitajaribu tena.
    Bin Zubeiry Sports – Online: Unaonekana una mwili mdogo na mabeki wengi wa kati wameshiba shiba, unawezaje kufunga dhidi yao                        
    Mbaraka Yussuf: Ukiwa na Malengo na ukijituma unaweza kufunga dhidi ya beki yoyote hata mwili nyuma 
    Bin Zubeiry Sports – Online: Nini Ndoto zako katika soka 
    Mbaraka Yussuf: Kufika mbali zaidi                        
    Bin Zubeiry Sports – Online: Una Meneja?                        
    Mbaraka Yussuf: Sina Meneja                        
    Bin Zubeiry Sports – Online: Nani sasa anakufanyia mipango ya kufika mbele                        
    Mbaraka Yussuf: Ndiyo natafuta       
    Bin Zubeiry Sports – Online: Baada ya kufunga goli ukiichezea timu ya taifa (Taifa Stars) kwa mara ya kwanza Machi 28, timu nyingi zimevutiwa na wewe hapa nchini, je upo tayari kuondoka Kagera?   Mbaraka Yussuf: Yah Nipo tayari kuondoka Kagera                        
    Bin Zubeiry Sports – Online: Huna mkataba unaokubana?
    Mbaraka Yussuf: Sina                        
    Bin Zubeiry Sports – Online: Na unataka dau gani kuondoka Kagera
    Mbaraka Yussuf: Hiyo ni siri yangu                        
    Bin Zubeiry Sports – Online: Mama yako yuko wapi  
    Mbaraka Yussuf: Yupo Tandika                        
    Bin Zubeiry Sports – Online: Anafanya shughuli gani  
    Mbaraka Yussuf: Mfanyabiashara                        
    Bin Zubeiry Sports – Online: Mpo watoto wangapi kwenu 
    Mbaraka Yussuf: Kwenye familia tupo wawili tu, mimi na mdogo wangu wa kike, anaitwa Hanifa      
    Bin Zubeiry Sports – Online: Umri wake                        
    Mbaraka Yussuf:  Miaka 16                        
    Bin Zubeiry Sports – Online: Anafanya nini kwa sasa yeye
    Mbaraka Yussuf: Yupo tu nyumbani  
    Bin Zubeiry Sports – Online: Niseme kwa leo inatosha. Asante sana ninakutakia kila la heri
    Mbaraka Yussuf Abeid: Asante sana kaka. Nawe pia
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBARAKA YUSSUF: CHIPUKIZI MWENYE NDOTO ZA KUFIKA MBALI KISOKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top