Arsene Wenger amemuambia Stan Kroenke atabaki Arsenal baada ya kumaliza mkataba wake wa sasa PICHA ZAIDI GONGA HAPA
KOCHA Arsene Wenger amemuambia mmiliki wa Arsenal, Stan Kroenke nia yake kutaka kuendelea kuwa kocha wa klabu hiyo.
Habari hizo zimeifikia bodi ya The Gunners katika kikao chake cha leo Jumanne.
Inamaanisha kwamba Wenger atasaini mkataba mpya wa miaka miwili.
Kroenke, aliyehudhuria fainali ya Kombe la FA Jumamosi Arsenal ikishinda 2-1 dhidi ya Chelsea Uwanja wa Wembley, London, amezungumza na Wenger zaidi ya saa 72 zilizopita.
Mfaransa huyo inafahamika amemuambia mwana hisa mkubwa wa klabu hiyo nia yake ya kubaki na Kroenke ndiye haswa anayemkingia kifua asing'oke.
0 comments:
Post a Comment