// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KAPOMBE ASITA KUONDOKA AZAM, AWAAMBIA SIMBA… - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KAPOMBE ASITA KUONDOKA AZAM, AWAAMBIA SIMBA… - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, May 31, 2017

    KAPOMBE ASITA KUONDOKA AZAM, AWAAMBIA SIMBA…

    Na Shekha Jamal, DAR ES SALAAM
    BEKI wa Azam FC, Shomary Kapombe amesema kwamba sasa bado hajafikiria kuondoka katika kikosi cha timu yake kutokana na mkataba kumbana.
    Kuna taarifa kwamba mchezaji huyo huenda akatua Simba kwa msimu ujao, kutokana na sera mpya za usukwaji mpya wa kikosi cha timu hiyo zilizosababisha pia, Nahodha wake John Raphael Bocco ‘Adebayor’ aondoke.
    Kapome ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online jana kwamba kwa sasa hawezi kuzungumzia suala la kurejea Simba, kwani bado ana mkataba wa muda mrefu na Azam.
    "Nina mkataba na Azam tena wa muda mrefu, hivyo kama Simba inanihitaji italazimika kwenda kwa viongozi wangu kukaa meza moja," alisema.
    Shomary Kapombe amesema kwamba hajafikiria kuondoka Azam kutokana na mkataba kumbana

    Kapombe alitua Azam FC msimu wa 2014 akitokea katika kikosi cha timu ya AS Cannes ya Ufaransa, ambayo nayo ilimchukua kutoka Simba kwa mkopo.
    Katika hatua nyingine, mdogo wake Shomary, Abbas Kapombe ni kati ya wachezaji watano wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Azam FC, waliopandishwa kikosi cha kwanza kwa ajili ya msimu ujao 2017-18.
    Wengine ni aliyekuwa wa U-20 ya Azam, Godfrey Elias, beki wa kulia Mohamed Omary, kiungo Stanslaus Ladislaus na mshambuliaji anayekuja kwa kasi Yahya Zaid.
    Ikumbukwe hata makipa Aishi Manula, Metacha Mnata, mabeki Ismail Gambo ‘Kussi’ na Gadiel Michael, nahodha msaidizi Himid Mao ‘Ninja’, Mudathir Yahya, Abdallah Masoud, mshambuliaji Shaaban Idd wote ni matunda ya program ya vijana ya Aza.
    Kikosi cha kwanza cha Azam kwa sasa kipo kwenye mapumziko ya wiki tano baada ya kumalizika kwa msimu na kitarejea tena mazoezini Julai 3 mwaka huu, kuanza maandalizi ya msimu mpya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAPOMBE ASITA KUONDOKA AZAM, AWAAMBIA SIMBA… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top