Kiungo wa Chelsea, Eden Hazard akiwa ameshika tuzo ya Bao Bora la Msimu usiku wa jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA
KIUNGO wa Chelsea, Eden Hazard ameshinda tena Tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu wa katika klabu hiyo katika sherehe zilizofanyika usiku wa jana mjini London.
Mbelgiji, ambaye pia ameshinda tuzo ya Bao Bora la Msimu katika sherehe zilizofanyika Battersea Evolution, huku N'Golo Kante akishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Wachezaji.
Kocha Antonio Conte alikabidhi tuzo hiyo kubwa, ambayo hutokana na kura za mashabiki baada ya kutolewa kwa orodha ya mwisho akiingia na Cesar Azpilicueta, David Luiz na Kante.
Usiku huo ukakamilishwa kwa sherehe ya kumuaga Nahodha John Terry anayestaafu, ambaye alipewa tuzo maalum kuutambua mchango wake.
Chelsea imemaliza msimu vizuri baada ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya England na kushika nafasi ya pili kwenye Kombe la FA.
0 comments:
Post a Comment