Kiungo wa timu ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, Abdul Suleiman akikosa bao la wazi baada ya kupiga mpira kutokea pembeni unaopitiliza upande wa pili kufuatia kumpita kipa wa Niger, Khaled Lawal Ibrahim jana katika mchezo wa mwisho wa Kundi B Fainali za Afrika Uwanja wa Port Gentil mjini Port Gentil, Gabon. Niger walishinda 1-0 na kufuzu Nusu Fainali huku Tanzania ikitolewa
Abdul Suleiman alianza kumpiga chenga vizuri beki wa Niger, Djibrilla Ibrahim Mossi
Lakini alipopiga mpira pamoja na kumpita kipa ukatoka nje na hakukuwa na mtu wa kuusindikiza nyavuni. Lilikuwa bao la wazi Serengeti walipoteza dakika za mwishoni jana


0 comments:
Post a Comment