Pierre-Emerick Aubameyang anatarajiwa kuondoka Borussia Dortmund kuhamia PSG ya Ufaransa PICHA ZAIDI GONGA HAPA
MSHAMBULIAJI wa Pierre-Emerick Aubameyang ataondoka Borussia Dortmund na kujiunga na Paris Saint-Germain kwa dau la Pauni Milioni 61 kwa mujibu wa taarifa kutoka Ufaransa.
Taarifa zimesema mshambuliaji huyo wa Gabon, ambaye amemaliza msimu kama mfungaji bora wa Bundesliga, amekubali mshahara wa Pauni 168,000 kwa wiki.
Pia imeelezwa kwamba, Aubameyang atapata kiasi cha Pauni Milioni 5.25 kama ada ya kusaini mkataba wa kujiunga na vigogo hao wa Ligue 1.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, ni mambo madogo tu ya kukamilishwa kabla ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 27 kuungana na Edinson Cavani na wenzake nchini Ufaransa.
Mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez imeelezwa naye ni mchezaji anayewaniwa pia PSG, lakini nyota huyo wa Chile anavutiwa zaidi na Manchester City na Bayern Munich.
Aubameyang amewaambia Dortmund anataka kuondoka baada ya kumakuza msimu akiisaidia timu yake kuifunga Eintracht Frankfurt 2-1 katika fainali Jumamosi na kutwaa Kombe la Ujerumani.
0 comments:
Post a Comment