// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ATUPELE GREEN ATUA SINGIDA UNITED MIAKA MIWILI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ATUPELE GREEN ATUA SINGIDA UNITED MIAKA MIWILI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, May 30, 2017

    ATUPELE GREEN ATUA SINGIDA UNITED MIAKA MIWILI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KLABU ya Singida United imefanikiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Atupele Green Jackson kutoka JKT Ruvu ya Dar es Salaam.
    Taarifa ya Singida United imesema mchezaji huyo amesaini mkataba wa miaka miwili usiku wa Jumatatu na Jumanne mchana anatarajiwa kutambulishwa rasmi.
    Atupele anajiunga na Singida United baada ya klabu yake, JKT Ruvu kushuka daraja katika msimu ambao alijiunga nayo kutoka Ndanda FC ya Mtwara.
    Atupele Green Jackson amejiunga na Singida United leo kwa mkataba wa miaka miwili

    Atupele ni mfungaji bora wa Kombe la Shirikasho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) mwaka jana, kabla ya mwaka huu kupokonywa na heshima hiyo na Mzambia, Obrey Chirwa wa Yanga.
    Na kumsajili Atupele ni mwendelezo wa Singida United kusajili wachezaji nyota wa nyumbani na nje ya nchi ili kutengeneza kikosi kikali cha ushindani msimu ujao.  
    Tayari Singida iliyopanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaye kocha mzoefu, Mholanzi Hans van der Pluijm iliyemchukua Yanga. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ATUPELE GREEN ATUA SINGIDA UNITED MIAKA MIWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top