KLABU ya Arsenal imempa ofa nyingine mshambuliaji wake, Alexis Sanchez aachane na mpango wa kwenda Bayern Munich na abaki Emirates.
Ofa mpya inaaminika itamfanya mchezaji huyo awe anapokea kiasi kisichopungua Pauni 270,000 kwa wiki, ambacho ni pungufu kidogo ya Pauni 300,000 alizoomba nyota huyo wa Chile.
Wakati kiasi hicho ni kidogo kulingana na kile alichoomba, mazungumzo zaidi yanatarajiwa kufanyika baada ya Arsenal kucheza na Chelsea kwenye fainali ya Kombe la FA Jumamosi.
Arsenal imempa ofa nyingine mshambuliaji wake, Alexis Sanchez aachane na mpango wa kwenda Bayern Munich na abaki Emirates PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment