MMAREKANI David Fields amethibitishwa kuwa refa wa pambano la ngumi za kulipwa uzito wa juu Jumamosi baina ya Anthony Joshua na Wladimir Klitschko.
Joshua, bingwa wa taji la IBF uzito mkubwa, atawania mataji yaliyo wazi ya WBA na IBO mwishoni mwa wiki Uwanja wa Wembley, London wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 90,000 wa kukaa.
Na siku hiyo bondia kipenzi cha Waingereza kwa sasa, Joshua atajaribu kuendeleza rekodi yake ya kutopigwa.
Na mzaliwa mzali huyo wa New Jersey, Fields atakuwa mtu mwingine ulingoni wakati wanaume hao wawili wanabadilishana mikono siku hiyo.
Fields amechezesha zaidi ya mapambano 200 katika kipindi chake cha miaka 17 ya kuwa refa wa ndondi, la karibuni zaidi likiwa la ushindi wa Ricky Lopez dhidi ya Pablo Cruz mjini New York mwezi Machi.
Itakuwa mara ya kwanza kwa refa huyo kufanya hiyo nchini Uingereza, kwani mapambano yake mengi yalifanyika Marekani.
Amewahi pia kuchezesha mapambano na ngumi katika nchi za Urusi, Japan, Ujerumani, Mexico, Canada na Afrika Kusini.
Pambano lingine pekee la uzito wa juu amewahi kuchezesha ni mwaka 2006 wakati Shannon Briggs anamshinda Chris Koval.
Pambano hilo lililofanyika ukumbi wa Hammerstein Ballroom in New York, won by Briggs katika raundi ya tatu, kuwania mataji yaliyokuwa wazi ya uzito wa juu ya USBA, WBO NABO na WBA-NABA.
Majaji watatu wa pamnano hilo ni Wamarekani Don Trella na Steve Weisfeld na Nelson Vazquez na Puerto Rico.
0 comments:
Post a Comment