MAGWIJI wawilli, Mmisri Wael Gomaa na Tresor Mputu Mabi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) watashiriki upangwaji wa makundi wa ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho inayotarajiwa kufanyika kesho makao makuu ya CAF, mjini Cairo, Misri.
Gomaa na Mputu ni majina makubwa katika miuchuano ya klabu Afrika, wakiwa wameshinda mataji na angalau klabu moja.
Mkongwe wa umri wa miaka 41, Gomaa, ambaye alistaafu mwaka 2014, ameshinda mataji sita ya Ligi ya Mabingwa na vigogo wa Misri, Al Ahly miaka ya 2001, 2005, 2006, 2008, 2012 na 2013 pamoja na ya Super Cup.
Tresor Mputu Mabi wa DRC atashiriki upangwaji wa makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho kesho mjini Cairo, Misri
Beki huyo mahiri alikuwemo kwenye kikosi cha kizazi cha dhahabu cha Ahly na wakali kama Essam El Hadary, Mohamed Aboutreika, Mohamed Barakat na Shady Mohamed ambacho kilitawala soka ya Afrika katika wakati huo.
Aliwika pia na kikosi cha timu ya taifa ya Misri akicheza Fainali tano za Kombe la Mataifa ya Afrika miaka ya 2002, 2004, 2006, 2008 na 2010 akishinda mataji matatu katika miaka ya 2006, 2008 na 2010.
Kwa upande wake, Mputu mwenye umri wa miaka 31 anaheshimika kama mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu katika zama zake.
Mfungaji bora kwenye michuano ya klabu barani Afrika, kwa mabao yake 43, anabaki kuwa mchezaji wa kipekee DRC na hususan katika klabu ya Lubumbashi, TP Mazembe, ambako anafanya kazi.
Alikuwa miongoni mwa wachezaji waliojengea heshima tena Mazembe miaka ya 2000 katikati akiwaongoza hadi kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2009 na Super Cup ya CAF mwaka huo huo.
Baada ya kucheza kwa muda mfupi, Kabuscorp ya Angola, akarejea kujiunga tena na Les Corbeaux’ mwishoni mwa mwaka 2016 na ameendelea kung'ara katika klabu hiyo.
Kiungo huyo mchezeshaji aling'ara pia kwenye michuano ya kwanza ya Ubingwa wa Mataifa wa Afrika (CHAN) nchini Ivory Coast ambako alichaguliwa Mchezaji Bora huku akiiwezesha DRC kushinda taji.
Wachezaji hao wawili watamsaidia Kaimu Katibu Mkuu wa CAF, Essam Ahmed kupanga droo hiyo ambayo itahudhuriwa na viongozi wa klabu zitakazoshiriki.

0 comments:
Post a Comment