Zlatan Ibrahimovic aliumia juzi Manchester United ikifuzu Nusu Fainali ya Europa League PICHA ZAIDI GONGA HAPA
MSHAMBULIAJI Zlatan Ibrahimovic anaweza kuwa nje ya Uwanja kwa sehemu yote ya msimu iliyobaki iwapo hofu ya maumivu ya goti lake la mguu wa kulia itathibitishwa.
Habari hizo zinaweza kuwa pigo kubwa kwa matumaini ya Manchester United kutwaa Kombe la Europa League na kumaliza kwenyw nafasi nne za juu katika msimamo wa Ligi Kuu ya England.
Msweden huyo amekuwa mshambuliaji kiongozi na tegemeo na ameweza kufunga mabao 28 katika msimu wake wa kwanza kwenye soka ya England.
Na pia itaweka shakani nafasi yake ya kuendelea kuichezea timu hiyo ya Old Trafford kwa msimu wa pili akiwa anaelekea kutimiza umri wa miaka 36 mwezi Oktoba.
Mapema wiki hii iliripotiwa Los Angeles ipo tayari kutoa ofa ya Pauni Milioni 5 kwa msimu kwa ajili ya mshambuliaji huyo na ofa yao bado ipo palepale na watafuraji Ibrahimovic akiandaliwa kisaikolojia kabla ya kuanza kucheza MLS.
Mkongwe huyo aliumia goti katika mchezo wa Robo Fainali ya Europa League Man United wakiitoa Anderlecht Alhamisi usiku.
Inahofiwa atakuwa amepata maumivu makubwa yatakayomuweka nje ya Uwanja kwa muda mrefu kati ya miezi sita hadi nane, hivyo kuwa amemaliza msimu na kukosa fainali ya Europa League itakayofanyika nchini kwao, Sweden mwezi ujao iwapo United itaitoa Celta Vigo.
Kinda Marcus Rashford anatarajiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji ya United katika mechi zilizosalia kuanzia dhidi ya Burnley kesho – baada ya kucheza vizuri na kuisaidia timu dhidi ya Chelsea na Anderlecht, na Wayne Rooney atarejea kazini.
0 comments:
Post a Comment