MSHAMBULIAJI Fernando Torres jana alikimbizwa hospitali nchini Hispania baada ya kuumia kichwani. Torres aliuamia baada ya kuingia dakika ya 65 akitokea benchi kuchukua nafasi ya Kevin Gameiro.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool na Chelsea, kwanza aliumia mapema tu katika mchezo wa Liga usiku wa jana dhidi ya Deportivo La Coruna Uwanja wa Manispaa ya Riazor mjini La Coruna, timu hizo zikitoka sare ya 1-1.
Aliangukia kichwa uwanjani baada ya kugongana na Alex Bergantinos na kuwashitua wachezaji wenzake baada ya hali yake kubadilika. Gabi alipigwa na Torres wakati akijaribu kumzuiaa asiueze ulimi.
Hata hivyo, Atletico Madrid imethibitisha mchezaji wake huyo anaendelea vizuri hospital.
Katika mchezo huo, Florin Andone alianza kuwafungia wenyeji dakika ya 13, kabla ya Antoine Griezmann kuisawazishia Atletico dakika ya 68.
Baadaye Torres mwenyewe akaandika kwenye akaunti yake Twitter kuwaambia mashabiki wasiwe na wasiwasi juu ya hali yake: "Asante nyingi kwa wote kwa kunifuatilia hali yangu na kwa meseji zenu za kunifariji. Ilikuwa ni hofu tu. Natumai kurejea karibuni!,".
0 comments:
Post a Comment