Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
SIMBA SC imepunguzwa kasi baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo, Simba inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 55, baada ya kucheza mechi 24, wakifuatiwa na mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 52 za mechi 23 ambao kesho watacheza ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Mbeya City wao baada ya sare leo, wanafikisha pointi 30 baada ya kucheza mechi 24.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Jacob Adongo wa Mara, hadi mapumziko Mbeya City walikuwa tayari mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na Ditram Nchimbi dakika ya 37 kwa shuti akimalizia kazi nzuri ya Raphael Daudi.
Shiza Kichuya ameifungia Simba bao la kusawazisha kwa penalti dakika ya 86
Pamoja na kutoka uwanjani ikiwa nyuma kwa bao 1-0, lakini Simba SC ndiyo waliotawala zaidi mchezo huo na kupoteza nafasi kadhaa nzuri za kufunga.
Beki wa kulia, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ alipiga shuti kali dakika ya 24, lakini kipa Mmalawi wa MCC, Owen Chaima akadaka na Nahodha Jonas Mkude naye alikaribia kuifungia Simba dakika ya 28 kama si shuti lake kwenda nje baada ya pasi ya winga Shiza Kichuya.
Mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo, Mrundi Laudit Mavugo alikaribia kufunga dakika ya 32 kama si beki wa Mbeya City, Rajab Zahir kuokoa.
Kiungo Muzamil Yassin alipiga shuti zuri baada ya krosi ya Hamadi Juma dakika 34, lakini mpira ukapaa juu na dakika ya 40 mshambuliaji mwingine tegemeo wa Simba, Ibrahim Hajib nusura aipatie bao timu yake kama si shuti lake kudakwa na Chaima.
Zaidi ya bao lao, shambulizi lingine la maana Mbeya City walifanya dakika ya 25, Ditram Nchimbi akipiga shuti kali baada ya pasi ya Bryson Raphael, lakini mpira ukaenda nje.
Hajib aliisawazishia Simba SC kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 65, uliopigwa nje kidogo ya boksi la Mbeya Ciry baada ya Bryson Raphael kuunawa mpira.
Baada ya bao hilo, Mbeya City wakafunguka na kuanza tena kusaka ushindi Uwanja wa ugenini na haikuwa ajabu walipofanikiwa kupata bao la pili dakika ya 79, mfungaji Nahodha wake, Kenny Ally.
Hata hivyo, Simba SC wakafanikiwa kusawazisha kupitia kwa Shiza Kichuya aliyefunga kwa penalti dakika ya 86 baada ya Tumba Lui kumuangusha beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kwenye boksi.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa: Daniel Agyei, Hamadi Juma, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, James Kotei, Abdi Banda, Jonas Mkude, Ibrahim Hajib/Mwinyi Kazimoto dk80, Muzamil Yassin/Mohammed ‘Mo’ Ibrahim dk54, Laudit Mavugo, Said Ndemla na Shiza Kichuya.
Mbeya City: Owen Chaima, Haruna Shamte, Majaliwa Shaaban, Tumba Lui, Rajab Zahir, Sankhani Mkandawile/John kabanda, Raphael Daudi, Kenny Ally, Ditram Nchimbi, Mrisho Ngassa/Ayoub Semtawa dk69 na Bryson Raphael/Zahor Pazi dk90.

0 comments:
Post a Comment