// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SAMATTA AFUNGA MAWILI GENK YAUA 5-2 ULAYA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SAMATTA AFUNGA MAWILI GENK YAUA 5-2 ULAYA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, March 10, 2017

    SAMATTA AFUNGA MAWILI GENK YAUA 5-2 ULAYA

    Na Mwandishi Wetu, GENK
    NYOTA ya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta imeendelea kung’ara baada ya usiku wa jana kufunga mabao mawili katika ushindi wa 5-2 kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 Bora UEAFA Europa League.
    Katika mchezo huo uliofanya Uwanja wa Ghelamco- Arena mjini Gent, Samatta alifunga mabao yake dakika za 41 na 72, wakati mengine ya wageni yalifungwa na kiungo wa Ukraine, Ruslan Malinovskiy dakika ya 21, mabeki Mgambia Omar Colley dakika ya 33 na Mfinland Jere Uronen dakika ya 45.
    Mbwana Samatta akipiga kifua kuwatambia wenyeji baada ya kuwatungua mabao mawili

    Samatta (kulia) na beki Mgambia Omar Colley wakisujudu baada ya kufunga jana

    Mabao ya wenyeji yalifungwa na mshambuliaji kutoka Nigeria, Samuel Kalu Ojim dakika ya 27 na mshambuliaji kutoka Mali, Kalifa Coulibaly dakika ya 61 na sasa Genk watakuwa na mchezo mwepesi wa marudiano nyumbani kuwania Robo Fainali.
    Samatta jana amefikisha mabao 16 katika mechi 47 alizoichezea Genk tangu asajiliwe Januari mwaka jana kutoka TP Mazembe ya DRC.
    Kati ya mechi hizo 47, michezo 18 Samatta alicheza msimu uliopita na 29 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 28 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 18 msimu huu.
    Mechi 19 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu, wakati 11 hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na tisa msimu huu na katika mabao hayo 16, 10 amefunga msimu huu na sita msimu uliopita.
    Kikosi cha KRC Genk jana kilikuwa: Ryan, Castagne, Brabec, Colley, Uronen, Berge, Malinovskyi/Heynen dk80, Pozuelo, Authors/Trossard dk90, Boetius/Buffalo dk45 na Samatta.
    KAA Gent: Kalinic, Gigot, Coulibaly, Matton, Mitrovic Saief/Simon dk76, Kalu, Perbet/Foket dk76 Verstraete/Rabiu dk45 Esiti na Gershon.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA AFUNGA MAWILI GENK YAUA 5-2 ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top