MSHINDI wa Kombe la Dunia, Kevin Grosskreutz amefukuzwa klabu ya Daraja la Pili Ujerumani, Stuttgart baada ya kupigwa katika ugomvi hadi kulazwa hospital.
Stuttgart imeandika katika tovuti kwamba beki huyo wa kulia mwenye umri wa miaka 28, mkataba wake umevunjwa baada ya tukio hilo.
Taarifa imeeleza umuhimu wa mchezaji wa kikosi cha kwanza kuwa mfano wa kuigwa katika klabu na kwamba Grosskreutz ameomba radhi kitendo alichokifanya.
Kevin Grosskreutz amesema kwamba hakutaka kitu cha namna hiyo kitokee katika soka yake. Na Grosskreutz binafsi yake akaomba radhi kwa kosa na kujutia namna anavyoondioka kwa fedheha Stuttgart.
Kevin Grosskreutz akijifuta machozi wakati anazungumza na Waandishi wa Habari kufuatia tukio hilo PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Nyota huyo wa zamani wa Borussia Dortmund hakuumia sana katika tukio hilo na Polisi walisema Jumanne kwamba alikimbizwa hospitali baada ya kupigwa ngumi katika mapigano baina ya makundi mawili Jumatatu.
Picha zilizowekwa Instagram zinaionyesha sura ya Grosskreutz ikiwa imevimba kwa kipigo na ina damu baada ya kipigo hicho.
Grosskreutz alikuwemo kwenye kikosi cha Ujerumani kilichotwaa Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil, ingawa hakucheza hata mechi moja kwenye mashindano hayo.
Alijiunga na Stuttgart kutoka Galatasaray, ambako hakufanikiwa kucheza kabisa baada ya mgogoro ulioibuka katika mkataba wake wa uhamisho kutoka Borussia Dortmund mwaka 2015.
0 comments:
Post a Comment