// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MTANZANIA WA UJERUMANI KUWANOA WENYE VIPAJI NCHINI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MTANZANIA WA UJERUMANI KUWANOA WENYE VIPAJI NCHINI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, March 29, 2017

    MTANZANIA WA UJERUMANI KUWANOA WENYE VIPAJI NCHINI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM 
    MTANZANIA anayeishi nchini Ujerumani Emanuel Austin, ameandaa mafunzo maalum ya kucheza muziki kwa vijana wa kitanzania wenye vipaji huku akitumia nafasi hiyo, kushauri wazazi na walezi kubaini vipaji vya watoto wao, tangu mapema. 
    Austin ametoa kauli hiyo Dar es Salaam leo ambapo anasema kwa nchini Ujerumani ana chuo ambacho kinatoa mafunzi ya kucheza muziki na kwa sababu anaipenda Tanzania, ameamua kutumia gharama zake kuja kutoa mafunzo hayo, ambapo kwa wanaohitaji usajili unafanyika kesho katika studio za Unleashead zilizopo Mikocheni B. 
    Mtanzania  anayeishi nchini Ujerumani  Emanuel Austin akizungumza na waandishi wa Habari,  Dar es Salaam Jana akizungumzia kufanyika kwa mafunzo ya siku moja ya vijana wenye vipaji vya kucheza muziki,  kwanza kulia Baba yake Mzazi Luis Austin wa Halali Moore na wakati wa kwanza kulia Msanii Ben Pol.          
    Austin ambaye yupo nchini ameambatana na baba yake Luis Auston, alisema pamoja na uamuzi wa siku nyingi wa kuona anatumia taaluma yake ya muziki kuisambaza kwa watazania pia msanii wa muziki wa kizazi kipya Bernad Paul 'Ben Pol' ndiyo amemuasasisha zaidi. 
    "Mimi nina chuo ninachofundisha uzeshaji wa muziki pia baba yangu nae anacho chuo ambacho kinafundisha muziki lakini pia ni kocha wa mpira wa miguu, hivyo Ben Pol ali[pokuja Ujerumani alifika kwenye vyuo vyetu na moja ya maombi yake kwetu alitaka tuje Tanzania ili kufundisha 
    uchezaji muziki na sasa tumekuja kwa ajili ya kazi hiyo"alisema. 
    Austin alisema kuwa, kuja kwake nchini Tanzania anategemea kuona vijana wengi kuja kujifunza kwani katika nchi za Ulaya watu wanaanza kujifunza mapema zaidi wakiwa na umri mdogo ndiyo maana wanaweza kufika mbali katika sekta mbalimbali. 
    Mkurugenzi Mtendaji wa Unleashed Academy Halila Mbowe amesema wanafuraha sana kuweza kuwakaribisha vijana katika kituo chao na pia kushirikiana na Emanuel Houston pamoja na Ben Pol kuja kuandaa mafunzo hayo kwa vijana. 
    Mbowe alisema  kuwa kituo chake kinajihusisha na masuala ya  kuinua vipaji katika kucheza mziki na kuandika mashairi na wameweza kupata vijana wengi na na takribani 25 tayari wameshaingia katika mashindano makubwa. 
    Baba yake na Emanuel, Luis Austin amesema kuwa alianza kukijua kipaji cha mwanae toka alivyokuwa mdogo na akamwambia kuwa utakuja kuwa mcheza mziki (dancer) na kweli mpaka sasa ameweza kuendesha maisha yake kupitia kucheza na ameshafungua kituo cha mafunzo nchini 
    Ujerumani na ana wanafunzi takribani 15000. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MTANZANIA WA UJERUMANI KUWANOA WENYE VIPAJI NCHINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top