GWIJI wa Liverpool, Ronnie Moran ‘Mr. Liverpool’ amefariki dunia leo asubuhi akiwa na umri wa miaka 83 baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, Paul Moran, gwiji huyo aliyeshinda mataji 44 na Liverpool ameacha simanzi kwa familia na jamaa.
Beki huyo wa zamani wa kushoto, aliichezea Liverpool mechi ya kwanza Novemba 1952 baada ya kujiunga nayo akitokea timu ya vijana ya Majogoo hao wa Jiji mwaka 1949 akiwa ana umri wa miaka 15 tu.
Katika mechi 379 alizochezea timu hiyo ya Anfield, Moran alifunga mabao 17 na mechi yake ya mwisho alicheza mwaka 1965 kabla ya kustaafu kucheza kandanda mwaka 1968 na akabakia klabuni hapo hadi mwaka 1999.
Ronnie Moran pamoja na mchango wake kama mchezaji, pia atakumbukwa kwa kitabu chake cha
Mr Liverpool kinachosimulia maisha yake na klabu yake.

0 comments:
Post a Comment