Na Princess Asia, DAR ES SALAAM TIMU ya Mlandizi Queens imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Taifa ya Wanawake baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Panama ya Iringa katika mchezo wa mwisho wa hatua ya Sita Bora ya michuano hiyo iliyodhaminiwa na Azam TV. Kwa ushindi huo, Mlandizi Queens ‘Watoto wa Mama Salma Kikwete’ wamemaliza na pointi 15, baada ya kucheza mechi tano na kuwapiku mahasimu wao, JKT Queens waliomaliza nafasi ya pili na Kigoma Stars nafasi ya tatu. Shujaa wa Mlandizi Queens leo alikuwa ni kiungo mshambuliaji wao hatari, Mwanahamisi Omar ‘Gaucho’ aliyefunga mabao manne peke yake katika dakika za kwanza, 35, 65 na 76 wakati bao lingine limefungwa na Fadhila Yussuf dakika ya 11.
Kiungo mshambuliaji wa Mlandizi Queens, Mwanahamisi Omar 'Gaucho' akimtoka beki wa Panama ya Iringa, Asha Malanda
Jamila Hassan Kassim akimtoma beki wa Panama
Beki wa Panama, Protosia Ngunda akipiga mpira dhidi ya mshambuliaji wa Mlandizi Queens, Rose Mpoma
Zainab Mlenda wa Mlandizi Queens akiondoka na mpira dhidi ya wachezaji wa Panama
Kikosi cha Mlandizi Queends kilichoanza leo
Timu nyingine zilizofuzu hatua ya Sita Bora ni Marsh Queens ya Mwanza iliyomaliza na pointi saba, Fair Play ya Tanga pointi tatu wakati Panama imemaliza bila pointi baada ya kufungwa mechi zote. Mlandizi Queens walistahili ushindi huu wa leo kutokana na kucheza vizuri mwanzo hadi mwisho na kwa ujumla, timu hiyo iling’ara tangu mwanzo wa Ligi Kuu ya ya Wanawake hatua ya makundi, inayofanyika kwa mara ya kwanza mwaka huu. Michuano hiyo ilianzia hatua ya makundi, Kundi A likiundwa na JKT, Mlandizi, Mburahati, Evergreen, Mtwara na Fair Play wakati Kundi B lilikuwa na Panama, Kigoma, Marsh, Bukoba Queens, Singida Queens na Dodoma Queens. Kikosi cha Mlandizi Queens kilikuwa; Janeth Simba, Zainab Mlenda, Shamira Makunguru, Hadija Mohammed, Wema Maile, Asfat Kasindo, Samira Hassan, Grace Mbelayi/Fatuma Issa dk47, Arafa Ramadhan/Rehema Buteme dk60, Mwanahamisi Omar ‘Gaucho’ na Fadhila Yussuf/Rose Mpoma dk72.
Panama Queens; Edina Ndelwa, Mariam Mbojela, Kapangala Kingamkono, Lucy London, Suzan Komba/Aidan Fukunyula dk84, Asha Malamwa, Eunice Tweve, Maimuna Mtoro/Margareth Luwokozo dk56, Antoneza Mbanga, Neema Nduye na Protosia Mbunda.
Bassett shines as Leicester beat Ulster to qualify
-
Josh Bassett scores a hat-trick as Leicester Tigers recover from a sloppy
start to beat Ulster and secure qualification for the knockout stage of the
Inves...
Media Accreditation for Uganda Vs Namibia
-
FUFA wishes to inform members of the sports media that the application
process for accreditation to cover the Women’s U17 World Cup Qualifier
match betwe...
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment