// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MALINZI KUFUNGA KOZI YA UKOCHA TANDIKA KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MALINZI KUFUNGA KOZI YA UKOCHA TANDIKA KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, March 12, 2017

    MALINZI KUFUNGA KOZI YA UKOCHA TANDIKA KESHO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi kesho Jumatatu, Machi 13, 2017 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya kufunga kozi ya ukocha ngazi ya kati kwa makocha 27 wanaotarajiwa kuhitimu.
    Kozi hiyo iliyoendeshwa na Wilfred Kidao - Mkufunzi anayetambuliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), itafungwa saa 5.00 asubuhi kwenye Viwanja vya Michezo vya Bandari, vilivyoko Tandika mjini Dar es Salaam.
    Jamal Malinzi kesho atafunga kozi ya ukocha ngazi ya kati mjini Dar es Salaam 

    Mbali ya Kidao, wakufunzi wengine walikuwa ni Manyika Peter aliyefundisha programu au mtaala kwa makocha wa makipa; Dk. Nassoro Ally Matunzya aliyewanoa makocha hao kuhusu tiba za wanamichezo/wanasoka na Mkufunzi wa muda mrefu wa soka, Hemed Mteza.
    Wanafunzi wa kozi hiyo wanaotarajiwa kuhitimu kesho Jumatatu ni pamoja Doris Malyaga ambaye ni Mwanamke pekee kati ya wanafunzi 27 walisoma kozi hiyo kwa kipindi cha siku 14 cha mwanzo wa mwaka.
    Wengine ni nyota wa zamani wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ waliopata kuchezea klabu kongwe na kubwa nchini. Wanafunzi hao ni Boniface Pawasa, Fred Mbuna, Innocent Haule, Herry Morris, Ivo Mapunda, Nizar Khalfan na Mussa Hassan Mgosi.
    Wengine ni Omar Kapilima, Amosi Mgisa, Uhuru Mwambungu, Yussuf Macho, George Minja, Haruna Adolf, Selemani Omari, Ally Ruvu, Masoud Selemani, Haji Mustapha, Mhasham Khatib, Issa Ndunje, Salum Kapilima, Said Salum, Julio Elieza, Hassan Mwakami, Rajab Mponda, Ally Mbonde na Evod Mchemba.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALINZI KUFUNGA KOZI YA UKOCHA TANDIKA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top