Luis Enrique anaamua kupumzika Barcelona baada ya miaka mitatu ya kufanya kazi klabu hiuyo ya Katalunya PICHA ZAIDI GONGA HAPA
KOCHA Luis Enrique ametangaza kuondoka Barcelona mwishoni mwa msimu huku kocha wa Everton, Ronald Koeman akiwa miongoni mwa wanaotarajiwa kumrithi.
Mholanzi huyo ataondoka miaka 25 baada ya ushindi wake wa Wembley kuipa Barcelona taji la kwanza kabisa la Ulaya.
Imekuwa siri ya wazi kwamba Enrique hataongeza mkataba mwishoni mwa msimu na ataondoka.
Uamuzi wa kocha huyo mwenye umri wa miaka 46 kutangaza sasa kuondoka kwake, ni kama kuwaambia wachezaji wake wajitume kumaliza msimu vizuri ili wagane kwa furaha.
"Nitamalizia mkutano huu na Waandishi wa Habari kwa namna tofauti, nataka kutangaza kwamba sitaendelea kuwa kocha wa Barcelona. Nataka kuishukuru klabu kwa imani yao yote waliyoonyesha kwangu. Hiyo imekuwa miaka mitatu ya kutosahaulika,"alisema jana baada ya ushindi wa 6-1 dhidi ya Sporting Gijon jana.
Ushindi huo umeirejesha Barca kileleni mwa La Liga, ikifikisha pointi 57 baada ya mechi 25 na kuashushia nafasi ya pili, Real Madrid yenye pointi 56 za mechi 24 sasa baada ya sare ya 3-3 na Las Palmas jana.
0 comments:
Post a Comment