Na Clement Shari, ARUSHA
KIINGILIO cha chini katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baina ya wenyeji, Madini FC na Simba SC kesho Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha kitakuwa ni Sh. 5,000.
Katibu wa Chama cha Soka Arusha (ARFA), Zakayo Mjema ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online jana kwamba maandalizi yote muhimu kuelekea pambano hilo yameshakamilika.
Mjema ametaja viingilio vingine kuwa ni Sh 20,000- VIP A, wakati wale watakaoketi VIP B1 na VIP B2 watalipa Sh 7,000 na Sh 5,000 itakuwa kwa jukwaa la VIP C1 na VIP C2.
Mjema amesema tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa siku ya Jumapili kuanzia saa moja
asubuhi Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na kwamba hakuna gari lolote litakaloruhusiwa kuingia uwanjani siku ya mchezo, hivyo wapenzi wa soka watakaokuwa na magari
watalazimika kutafuta maegesho nje ya Uwanja.
Timu hizi zinakutana kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya soka la Tanzania, Madini wanashiriki Ligi Daraja la Pili wakati Simba ni vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa sasa.

0 comments:
Post a Comment