Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
TIMU tano zimefuzu hatua ya sita bora ya Ligi ya Wanawake Tanzania Bara baada ya hatua ya makundi, wakati mechi za mwisho zitaamua timu ya mwisho ya kukamilisha hatua hiyo.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas ameiambia leo Bin Zubeiry Sports – Online kwamba kutoka Kundi B timu zote tatu za kusonga sita bora zimekamiliaa mbazo ni JKT Queens ya Dar es Salaam, Mlandizi Queens ya Pwani na Fair Play ya Tanga.
Timu zilizikosa nafasi ya kusonga mbele kutoka kundi hilo ni Evegreen ya Temeke, Mburahati Queens ya Dar es Salaam na Viva ya Mtwara.
Lucas alisema timu zilizofuzu hadi sasa kutoka Kundi A ni Sisters ya Kigoma na Marsh Academy ya Mwanza. Timu nyingine zilizobaki ambazo zinawania nafasi moja ya kukamilisha timu za kufuzu Sita Bora kutoka kundi hilo ni Panama ya Iringa, Baobab ya Dodoma, Majengo ya Singida na Victoria na Queens ya Kagera.
Hatua ya Sita Bora inatarajiwa kuanza katikati ya mwezi Uwanja wa Karume, Dar es Salaam na bingwa atajainyakulia Kombe na Medali za rangi ya Dhahabu, mshindi wa pili Kombe na Medali za rangi ya Fedha.

0 comments:
Post a Comment