// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); OMOG AMTUPA JUKWAANI MWANJALI, AWAANZISHA LUFUNGA NA BANDA BEKI YA KATI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE OMOG AMTUPA JUKWAANI MWANJALI, AWAANZISHA LUFUNGA NA BANDA BEKI YA KATI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

        Saturday, February 25, 2017

        OMOG AMTUPA JUKWAANI MWANJALI, AWAANZISHA LUFUNGA NA BANDA BEKI YA KATI

        Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
        KOCHA Mcameroon wa Simba, Joseph Omog amemuondoa kabisa Method Mwanjali katika programu ya mchezo wa leo dhidi ya Yanga.
        Watani hao wa jadi katika soka ya Tanzania wanamenyana kuanzia Saa 10:00 jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.   
        Mwanjali aliumia katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Prisons Februari 11 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na pamoja na jitihada za kumfanya arejee kwa ajili ya mchezo wa leo, imeshindikana.
        Kwa sababu huyo, Omog amewaanzisha pamoja katika beki ya kati Novaty Lufunga na Abdi Banda, huku pembeni wakichezeshwa Janvier Besala Bokungu kulia na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kushoto.
        Method Mwanjali yupo jukwaani kabisa leo akidhuhudia Simba yake ikimenyana na Yanga

        Kwa ujumla kikosi cha Simba SC kinachoanza ni; Daniel Agyei, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Abdi Banda, James Kotei, Ibrahim Hajib, Muzamil Yassin, Juma Luizio, Laudit Mavugo na Mohammed ‘Mo’ Ibrahim.
        Katika benchi wapo; Peter Manyika, Jonas Mkude, Hamad Juma, Said Ndemla, Shiza Kichuya, Mwinyi Kazimoto na Pastory Athanas. 
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: OMOG AMTUPA JUKWAANI MWANJALI, AWAANZISHA LUFUNGA NA BANDA BEKI YA KATI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry