Na Mwandishi Wetu, KAHAMA
KIKOSI cha Mbeya City Fc kimeweka kambi Kahama tangu juzi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Stand United kesho Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Mbeya City imejificha Kahama ikitokea Mwadui, ambako mwishoni mwa wiki ilifungwa 3-2 na wenyeji, Mwadui FC katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu na sasa wanalekekeza nguvu zao kwenye mchezo wa kesho.
Mchezaji nyota wa Mbeya City, Mrisho Ngassa kesho anatarajiwa kuisaidia timu yake dhidi ya Stand United
Kocha Msaidizi wa Mbeya City, Mohamed Kijuso alisema jana kwamba kulikuwa na makosa kadhaa kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mwadui FC jambo lililosababisha kufungwa mabao mawili ya haraka haraka na hatimaye kumaliza dakika 90 City ikiwa imepoteza mchezo huo wa ugenini kwa bao 3-2.
"Kwa vyovyote tunalazimika kusaka matokeo kwenye mchezo ujao, tulikuwa na makosa mengi mchezo uliopita, tumesafiri mpaka hapa Kahama kuweka kambi ya siku nne lengo letu likiwa ni kupata utulivu wa kujiandaa vizuri na mchezo wa Ijumaa dhidi ya Stand United,"alisema.

0 comments:
Post a Comment