Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MARA baada ya wiki iliyopita Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuipongeza timu ya Lipuli ya Iringa, leo Jumanne Februari 21, mwaka huu kwa mara nyingine, Rais wa TFF Jamal Malinzi amezipongeza kwa mpigo, timu za Singida United ya Singida na Njombe Mji ya Njombe kwa kupanda daraja.
Juma lililopita, Rais Malinzi aliuandikia barua uongozi wa Lipuli ya Iringa kwa mafanikio ya kupanda daraja msimu huu kutoka Ligi Daraja la Kwanza hadi Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2017/18 kama alivyofanya sasa kwa Singida United ya Singida na Njombe Mji ya Njombe.
Nizar Khalfan ni mmoja wa wachezaji walioipandisha Singida United
Katika salamu hizo kwa Lipuli ambayo imepanda daraja baada ya kusota miaka 17 iliposhuka daraja, Rais Malinzi alimwandikia barua Katibu Mkuu wa timu hiyo akisema: “Nitumie fursa hii kukupongeza wewe, uongozi wa klabu yako, benchi la ufundi na wadau wote wa timu ya Lipuli kufuatia kupanda daraja kwenda Ligi Kuu.
Kama ilivyotokea kwa Lipuli, Rais Malinzi pia kwa moyo mkunjufu amewaandikia barua, viongozi wa Singida United ya Singida na Njombe Mji ya Njombe, akisema: “Pia nanyi nawapongeza kwa kupanda daraja. Bila shaka ni kazi kubwa imefanyika ikihusisha kujitolea kwa ari na mali kuhakikisha mnafika hapa mlipo.”
Pamoja na salamu hizo za kuwapongeza, Rais Malinzi hakuacha kuziusia timu hizo akisema: “Rai yangu kwenu ni kuongeza juhudi na kuendesha klabu kwa weledi mkubwa zaidi ili muweze kuwa washindani wa kweli katika ligi (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara).”

0 comments:
Post a Comment