KIUNGO Frank Lampard ametangaza kustaafu soka ya ushindnai baada ya zaidi ya miongo miwili ya kuwa kazini.
Gwiji huyo wa Chelsea, ambaye alishinda heshima zote kubwa wakati wake akiwa kazini Stamford Bridge, ameamua kustaafu baada ya kuondoka New York City ya Ligi Kuu ya Marekani mwishoni mwa msimu.
Lampard, mwenye umri wa miaka 38 sasa, ametangaza kustaafu kwake kupitia ukurasa wake wak Instagram ambako ameposti ujumbe wa kuwashukuru wote waliochangua mafanikio yake ikiwemo kuichezea mechi 106 timu yake ya taifa ya England.
Kiungo wa zamani wa Chelsea na England ametangaza kustaafu soka PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Lampard ameishukuru familia yake, akiwemo mkewe Christine ambaye ameandika ujumbe wa kujivunia mumewe kwenye ukurasa wake wa Instagram pamoja na picha ya 'bwana mkubwa huyo'.
Lampard amezishukuru pia klabu alizochezea enzi zake kuanzia West Ham katikati ya miaka tisini. Amesema Chelsea, ambako ameshinda mataji matatu ya Ligi Kuu ya England, mannde ya FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya zaidi ya miaka 13 daima itabakia kuwa na nafasi kubwa moyoni mwake na pia akazishukuru Manchester City na New York City.
0 comments:
Post a Comment