Wachezaji wa Ngaya de Mde ya Comoro wakiwa wameshika mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa (katikati) baada ya kwenda kutoa sarafu kwenye lango lao wakati wa mchezo wa marudiano baina ya timu hizo Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hizo zimetoka sare ya 1-1 na Yanga imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 6-2 baada ya wiki iliyopita kushinda 5-1 ugenini mjini Moroni, Comoro.
Chirwa alipambana asipokonywe sarafu hiyo
Wachezaji wa Ngaya walijitahidi kumpokonya sarafu hiyo bila mafanikio
Lakini hawakukata tamaa, walihakikisha wanamdhibiti vizuri ili aiachie
Alipoona anakaribia kuzidiwa nguvu, Chirwa akaitupa nje sarafu hiyo
Baada ya kuitupa nje akaamini sasa ugumu wa kupata mabao utaisha
Hapa anawaambia; "Sarafu yenu inaayotuzuia tusiwafunge mabao ilee" pichani chini
Duke's Jon Scheyer: Cooper Flagg Made 'Zion Kind of Play' on Viral Dunk vs.
Pitt
-
The Duke men's basketball team defeated Pittsburgh 76-47 on Tuesday, but it
was one play that stood out more than the final score. Freshman Cooper
Flagg st...
42 minutes ago
0 comments:
Post a Comment