Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeamuru mchezo wa Raundi ya Nne ya Kombe la Azam Sports Federeation Cup HD (ASFC) kati ya Mighty Elephant na Shujaa ya Kigoma urudiwe Jumatano
Hatua hiyo inafuatia TFF kuikubali rufaa ya timu ya Shujaa kupinga Mighty Elephant kupewa ushindi wa mezani.
Shujaa haikutokea kwenye mchezo dhidi ya Mighty Elephant Uwanja wa Maji Maji mjini Songea na wapinzani wao wakapewa ushindi wa mezaji, hivyo kupangwa kumenyana na Maji Maji ya Songea juzi katika Raundi ya Tano.
Maji Maji sasa itasubiri mshindi kati ya Mighty Elephant na Shujaa ya Kigoma watakaomenyana Jumatano
Hata hivyo, saa chache kabla ya kufanyika mchezo kati ya Maji Maji na Mighty Elephant juzi Uwanja wa Maji Maji, TFF ikaufuta mchezo huo.
Na lengo ni kutaka Might Elephant imenyane kwanza na Shujaa na mshindi ndiye atakwenda kucheza na Maji Maji.
Michuano ya Kombe la ASFC inatarajiwa kuendelea leo kwa Stand United kuwa wageni wa Polisi Mara Uwanja wa Karume, Musoma, Azam FC na Cosmopolitan Uwanja wa Azam Complex, Chamazi na Ndanda FC dhidi ya Mlale JKT Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

0 comments:
Post a Comment