Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo miwili kwenye viwanja viwili tofauti nchini.
Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, wenyeji African Lyon wataikaribisha JKT Ruvu mchezo ambao awali ulipangwa kufanyika jana na Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Toto Africans wataikaribisha Stand United ya Shinyanga.
Kocha wa JKT Ruvu, Bakari Shime alisema jana kwamba baada ya vijana wake kupoteza mechi mbili zilizopita mbele ya Yanga na Simba, leo watapaswa kupigana kiume washinde.
Shime alisema kwamba kwa kitambua JKT wapo kwenye nafasi mbaya katika msimamo wa Ligi Kuu, basi wamekubaliana na kupigana kiume kupata matokeo mazuri kuanzia sasa.
Kwa upande wake, Meneja Toto Africans, Khalfan Ngassa alisema kwamba baada ya sare ye ugenini na Mbeya City mjini Mbeya, vijana wake wamerejea na nguvu mpya mjini Mwazna kwa ajili ya kuwafunga Stand United.
“Mimi ninafahamu Stand United ni wazuri na mzunguko wa kwanza walifanya vizuri, lakini sisi tumejipanga vyema kuwafunga,”alisema Ngassa.

0 comments:
Post a Comment