Na Mwandishi Wetu, MBEYA
BAADA ya ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Kabela City FC ya Shinyanga kwenye kombe la FA hapo jana, kikosi cha Mbeya City Fc leo kimeanza mazoezi kujindaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya Tanzania Prison uliopangwa kuchezwa mwishoni mwa juma hili kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa.
Kocha Msaidizi wa kikosi hiki Mohamed Kijuso amesema kwamba maandalizi kuelekea mchezo huo wa Jumamosi yanaenda vizuri na wachezaji wote wako kwenye hali nzuri, kinachofanyia sasa ni kurekebisha makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo wa kombe la FA licha ya kupatikana kwa ushindi wa bao 2-0.
"Tunashukuru Mungu kwa sababu tulipata matokeo kwenye mchezo wa kombe la FA hapo jana licha ya mchezo kuwa mgumu, tuko mazoezini hivi sasa kurekebisha makosa yote yalitokea hii ni sehemu ya maandalizi yetu kuelekea mchezo ujao,"alisema.
Kijuso aliongeza kuwa kwa mujibu wa daktari, vijana wachezaji wote wapo fiti kuelekea mchezo huo. "Ninaiheshimu Tanzania Prison ni timu nzuri huwezi kuibeza kwa namna yoyote, ni wazi mchezo wa jumamosi utakuwa mgumu,".
Akiendelea zaidi Kijuso alisema kuwa mipango na malengo ya kikosi chache ni kuhakikisha wanakuwa sehemu ya timu nne za juu kwenye msimamo wa ligi mara ifikapo mwisho wa msimu.
Mara kadhaa nimekuwa nikisema nia yetu ni kuwa sehemu ya timu nne za juu mwisho wa msimu,hili litawezekana kwa sababu nafasi bado tunayo, nina imani kubwa na vijana wangu kwa sababu sasa wako kwenye kiwango kizuri, kitu pekee naomba mashabiki wetu watusapoti kwa nguvu zote kama ambavyo wamekuwa wakifanya kwenye michezo iliyopita.

0 comments:
Post a Comment