KLABU ya Liverpool haijataka kupoteza muda zaidi kumrejesha mchezaji wake tegemeo, Sadio Mane kutoka kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.
Mane alikosa penalti ya mwisho jana Senegal ikitolewa na Cameroon kwenye Robo Fainali ya AFCON kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 0-0.
Na wamiliki wa Liverpool, Fenway Sports Group, wamemuandalia ndege maalum binafsi mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 arejee haraka England.
Mane anatarajiwa kurejea moja kwa moja kwenye kikosi cha Wekundu hao kwa ajili ya mchezo wa Jumanne dhidi ya vinara, Chelsea.
Liverpool imemkodia ndege Sadio Mane arejee haraka kutoka Gabon
Amechukua ndege binafsi kutoka Gabon na anatarajiwa kuwa benchi kama mchezaji wa akiba siku hiyo.
Hii si mara ya kwanza kwa wamiliki wa Liverpool kuwakodia ndege wachezaji, kwani Novemba mwaka 2013, walimtumia ndege Luis Suarez arejee kutoka kwenye mechi ya kufuzu Kombe la Dunia Amerika Kusini kwa ajili ya mchezo wa mahasimu wa Merseyside Uwanja wa Goodison Park. Na Suarez akafunga kwenye mchezo huo.
Liverpool pia ilikodi ndege kwa mechi dhidi ya PSG na Chelsea ili kuwapata mapema wachezaji wake wa Kibrazil kutoka Amerika Kusini Novemba. Na mashabiki wa Liverpool watafurahia kurejea kwa mchezaji huyo, kutokana na timu hiyo kushinda mechi moja tu katika kipindi ambacho hakuwapo.
Kikosi cha Jurgen Klopp kimekuwa na mwezi mgumu wa Januari baada ya kutolewa kwenye mashindano yote, Kombe la Ligi na Kombe la FA na kupoteza mwelekeo piaa kwenye Ligi Kuu ya England.
Walifungwa 2-1 na timu ya Daraja la Kwanza, Wolves Jumamosi kwenye Raundi ya Nne ya Kombe la FA.
0 comments:
Post a Comment