// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KIKOSI CHA OLIMPIKI KUINGIA KAMBINI JUMAPILI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KIKOSI CHA OLIMPIKI KUINGIA KAMBINI JUMAPILI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, January 26, 2017

    KIKOSI CHA OLIMPIKI KUINGIA KAMBINI JUMAPILI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 23 ‘Kilimanjaro Warriors’ inatarajiwa kuingia kambini Janauri 29, 2017 kwa ajili ya maandalizi ya awali ya kucheza mechi za kufuzu fainali za Olimipiki zitakazofanyika jijini Tokyo, Japan mwaka 2020.
    Kambi hiyo ya wiki moja itafanyika kwenye Hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambako pia kuna Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazoezi kulingana na program za walimu.
    Tanzania haijapata kushiriki Michuano ya Olimpiki kwa upande wa mpira wa miguu jambo ambalo limeisukuma TFF kuona kuwa ni fursa ya mpira wa miguu kuchezwa hivyo inashirikiana na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), kufanikisha mipango na taratibu.
    Tanzania kwa sasa ina vijana wengi waliotokana na michuano ya Mradi wa kuibua na kukuza vipaji wa Airtel kadhalika na Cocacola ambao wamekuwa chachu ya maendeleo ya timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys.
    Vijana hawa wa Airtel, Copa Coca Cola na Serengeti Boys wataungana na baadhi ya vijana waliofanya vizuri kwenye Ligi ya Vijana wenye umri wa chini miaka 20 kutoka timu za Ligi Kuu ambao wamezaliwa baada ya tarehe 1 Januari 1997 ili kuunda kikosi imara cha awali kuelekea kufuzu kwa michuano ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo Japan, mwaka 2020.
    Kwa kufuata utaratibu wa maandalizi ya Serengeti Boys na kwa kushirikiana na TOC timu hii itapewa mazoezi na michezo  ya kujipima nguvu ndani na nje ya nchi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIKOSI CHA OLIMPIKI KUINGIA KAMBINI JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top