Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
WACHEZAJI wa Yanga kwa siku ya pili leo wameendelea na mgomo kufanya mazoezi wakishinikiza walipwe mishahara yao ya Novemba.
Ni wachezaji wawili tu walioonekana Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam asubuhi ya leo, kipa Ally Mustafa ‘Barthez’ na beki Oscar Joshua.
Zaidi ya hapo walitokea makocha tu, George Lwandamina na Wasaidizi wake, Noel Mwandila Mzambia mwenzake na wazalendo, Juma Mwambusi, kocha wa makipa Juma Pondamali, Meneja Hafidh Saleh, Daktari Edward Bavu, Mchua Misuli Jacob Onyango na Mtunza Vifaa Mohammed Omar ‘Mpogolo’.
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit alifika Uwanja wa Uhuru na kukutana na hali hiyo ya kushangaza na akaenda kuzungumza na Lwandamina baadaye Mwambusi na Hafidh.
Baada ya hapo wote wakaondoka na leo asubuhi mazoezi hayakufanyika Yanga.
Mgomo huo ulianza ghafla jana baada ya wachezaji kufika Uwanja wa Uhuru jioni, lakini wakagoma kuingia uwanjani kufanya mazoezi.
Uongozi wa Yanga umekanusha kuwapo kwa madai ya mishahara ya Novemba na kwamba wachezaji wanagoma wakitaka walipwe mapema mishahara ya mwezi huu, Desemba.
“Kinacholeta matatizo hapa ni kubadilika kwa mfumo wa ulipaji, yaani badala mwishoni mwa mwezi, sasa tunalipa mwanzoni mwa mwezi. Sasa wachezaji wanataka mishahara ya Desemba walipwe mapema kwa sababu ya hizi sikukuu,”alisema Baraka akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo.
Taarifa zaidi zinasema kwamba kutakuwa na kikao mchana wa leo kati ya wachezaji na viongozi wa Yanga kulitafutia ufumbuzi suala hilo.
Mgomo huu unakuja wakati Yanga ipo katika maandalizi ya mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya African Lyon Ijumaa wiki hii Uwanja wa Uhuru.

0 comments:
Post a Comment