// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); STRAIKA WA NDANDA AWA MCHEZAJI BORA WA NOVEMBA LIGI KUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE STRAIKA WA NDANDA AWA MCHEZAJI BORA WA NOVEMBA LIGI KUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, December 03, 2016

    STRAIKA WA NDANDA AWA MCHEZAJI BORA WA NOVEMBA LIGI KUU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI Riphat Hamisi wa timu ya Ndanda FC amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Novemba kwa msimu wa 2016/2017.
    Riphat ambaye ni mshambulaji aliwashinda wachezaji Shaban Idd wa Azam FC na Mbaraka Abeid wa Kagera Sugar.
    Katika mechi mbili ambazo timu ya Ndanda FC ilicheza kwa mwezi huo, Riphat aliisaidia timu yake kupata ushindi katika michezo yote na kukusanya jumla ya pointi 6 zilizoifanya kushika nafasi ya kumi katika msimamo wa Ligi hiyo ambayo iko mapumzikoni kupisha dirisha dogo la usajili.
    Aliifungia pia timu yake mabao mawili katika michezo miwili ambayo timu yake ilicheza kwa mwezi huo.
    Mwezi huo ulikuwa na raundi mbili zilizochezwa. Kwa kushinda tuzo hiyo, Riphat atazawadiwa kitita cha sh. milioni moja kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STRAIKA WA NDANDA AWA MCHEZAJI BORA WA NOVEMBA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top