Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TIMU ya Simba imefanikiwa kuingia fainali ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, baada ya kuitoa kwa penalti 8-7 Stand United ya Shinyanga katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam jioni ya leo.
Katika mikwaju tisa, Simba walipoteza mmoja na Stand wakapoteza miwili baada ya dakika 120 za timu hizo kufungana bao 1-1 kwenye mchezo safi na wa kuvutia.
Waliofunga penalti za Simba ni Calvin Faru, Mokiwa Perus, Rashid Juma, Vicent Costa, Moses Kitandu, George Emanuel na Adnan Ayoub wakati Mohammed Mussa alikosa.
Wachezaji wa Simba wakishangilia baada ya ushindi wa penalti 8-7 dhidi ya Stand United ya Shinyanga leo katika Nusu Fainali ya Ligi Kuu ya Vijana
Kwa upande wa Stand United waliofunga ni Adam Salamba, Vitalis Mayanga, Said Ally, Omari Kanyoro, Suleiman Mrisho, Rajab Seif na Hassan Yassin, wakati Msenda Amri na Fahmay Mahmoud walikosa.
Awali, Simba ndiyo waliotangulia kupata bao lililofungwa na Hussein Hamisi dakika ya 19 kwa shuti kali baada ya pasi ya Rashid Juma, kabla ya Stand kusawazisha kupitia kwa Adam Salamba dakika ya 53 kwa kwaju wa penalti baada ya beki mmoja wa Simba kuunawa mpira kwenye boksi.
Sasa Simba wanaingia fainali ya Ligi Kuu ya kwanza ya vijana inayokuja kwa udhamini wa Azam TV na watakutana na mshindi kati ya Azam FC na Mtibwa Sugar zinazomenyana katika Nusu Fainali ya pili.
Kikosi cha Simba kilikuwa; Athumani Nyamaka/Ally Salim dk61, Calvin Faru, Joseph Anthony, Mokiwa Perus, Adnan Ayoub, Hussein Hamisi/Mohammed Mussa dk67, George Emanuel, Moses Kitandu, Ally Abdallah/Said Hamisi dk61 na Rashid Juma.
Stand United: Thomas Matola, Alphonce Ezekiel, Brown Nicolous, Fahmy Mohmoud, Rajab Seif, Suleiman Mrisho, Abel Yegela, Vitalis Mayanga, Adam Salamba, Omary Kanyoro na Stanley Angelo/Msenda Amri dk75.

0 comments:
Post a Comment