MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo ndiye nyota mpya anayetakiwa Ligi Kuu ya China na wakala wake, Jorge Mendes ametaja dau alilotengewa kijana wake.
Kwa mujibu wakala huyo babu kubwa, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31amepewa ofa mkataba wa malipo ya Pauni Milioni 1.6 kwa wiki kutoka klabu ya CSL, ambayo pia ipo tayari kuilipa Real Madrid dau la rekodi la uhamisho, Pauni Miloni 260.
Pamoja na hayo, mbele ya mshindi wa tuzo nne za Ballon d'Or inatokea kwamba fedha, au fedha nyingi si kitu kwake na Mendes amesema Ronaldo tayari ameikataa ofa hiyo.
"China wametoa ofa ya Euro Milioni 300 (Pauni Milioni 260) kwa Real Madrid na zaidi ya Euro Milioni 100 (Pauni Milioni 85) kwa mwaka kwa mchezaji. Lakini fedha si kila kitu; Klabu ya Hispania ndiyo maisha yake,".
Ronaldo amekataa Pauni Milioni 1.6 kwa wiki kujiunga na klabu ya CSL
Shanghai SIPG tayari imemnunua kwa Pauni Milioni 60 Oscar kutoka kikosi cha Antonio Conte cha Chelsea, na wapinzani wao Jiji, Shanghai Shenhua wamemchukua Carlos Tevez na kumfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi duniani, Pauni Milioni 615,000 kwa wiki.
Kwa mujibu sa jarida la Forbes, akikusanya mapato yake yote ya mwaka, Ronaldo anaingiza fedha nyingi zaidi ya mchezaji mwingine yeyote duniani na kwa makadirio anaingiza Pauni Milioni 71 kwa mwaka.
Na thamani imezidi kukua mwaka 2016 baada ya kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Uaya na Real Madrid kabla ya kushinda Kombe la Euro na Ureno, mafanikio ambayo yalimfanya ashinde Ballon d'Or ya nne na anatarajiwa pia kupewa tuzo ya Mchezaji Bora wa Kiume wa FIFA dhidi ya wapinzani wake, Lionel Messi na Antoine Griezmann Januari mwakani.
Oscar naa Tevez wataungana na wachezaji wengine wanaolipwa vizuri China kama Hulk na Graziano Pelle wakati Nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney anabakia kuwa mchezaji anayetakiwa sana huko.
Zlatan Ibrahimovic alikataa ofa ya mshahara wa Pauni Milioni 1 kwa wiki mwanzoni mwa msimu na kuamuaa kwenda Old Trafford.
0 comments:
Post a Comment