HABARI mbaya kwa Arsenal ni kwamba, imethibitika kiungo tegemeo Santi Cazorla atakwenda kufanyiwa upasuaji ambao utamfanya akose sehemu kubwa ya harakati za klabu yake kuwania taji.
Mchezaji huyo wa Hispania alipigwa kwenye kifundo cha mguu wake wa kulia katika mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Ludogorets Oktoba 19, mwaka huu na kuumia.
The Gunners wamejitahidi kufanya kila namna kumuepusha na kufanyiwa upasuaji, lakini uamuzi sasa umetolewa kwamba Cazorla, ambaye alizuru kwa wataalamu wa Hispania kwa ajili ya tatizo lake, atakwenda kufanyiwa upasuaji.
Kiungo wa Arsenal, Santi Cazorla atakuwa nje kwa miezi mitatu kutokana na maumivu ya mguu wa kulia yanayohitaji upasuaji
Kukosekana kwa Cazorla ni pigo kubwa kwa kocha Arsene Wenger kwa sasa Arsenal akiwa kwenye harakati za kuwania taji la kwanza la Ligi Kuu ya England baada ya muda mrefu.
Hiyo ni kwa sababu kiungo huyo amekuwa akiiunganisha vizuri timu kwa pasi zake maridadi kutoka kwenue ulinzi hadi ushambuliaji.
Na wachezaji wenzake wameshinda mechi mbili tu za Ligi Kuu tangu Cazorla aumie. Cazorla atasafiri kwenda Sweden wiki ijayo kufanyiwa upasuaji na anatarajiwa kuwa nje si kwa zaidi ya miezi mitatu.
0 comments:
Post a Comment