Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
NUSU fainali ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20, inafanyika kesho Novemba 9, kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Mbagala-nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Hatua hiyo itazikutanisha timu za Azam FC ya Dar es Salaam na Mtibwa Sugar ya Dar es Salaam katika mchezo utakaoanza saa 10.00 (16h00) kabla ya nusu fainali ya pili itazikutanisha timu za Simba ya Dar es Salaam na Stand United ya Shinyanga katika mchezo utakaofanyika kuanzia saa 1.00 )usiku (19h00).
Simba ilifikia hatua hiyo baada ya kuibuka kinara katika kundi A la michuano hiyo ambako ilifikisha pointi 17 na kuzishinda nyingine saba kama ilivyotokea kwa Azam FC ambayo pia ilifikisha pointi 17 katika kundi B ambalo kituo chake kilikuwa Kagera.
Michuano hiyo iliyochezwa kwa udhamini wa Azam Tv na Benki ya DTB yaani Diamond Trust Benk, iliziibuka Mtibwa Sugar ambayo ilishina nafasi ya pili kwa kituo cha Dar es Salaam kwa kujikusanyia pointi 14 kama ilivyotokea kwa Stand United ambayo pia ilishika nafasi ya pili katika kituo cha Dar es Salaam.

0 comments:
Post a Comment